| Viongozi wa UKAWA wakizungumza na waandishi wa habari |
Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA nchini Tanzania, wamesema kuwa, wamemwandikia barua Spika wa Bunge la nchi hiyo, Job Ndugai vikitaka kujua uhalali wa Rais John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge kabla ya kutangazwa matokeo rais wa Zanzibar. Katika mkutano wao na waandishi wa habari mapema leo, viongozi wa umoja huo wamesema kuwa, hawatakubali Rais Magufuli ahutubie bunge hilo la 11, ilhali hatima ya Rais wa Zanzibar bado haijajulikana, kama ambavyo pia wamesisitiza kuwa, hawataruhusu Dk Shein kuingia bungeni wakati muda wake wa kushika madaraka umeshapita.
Wakati huo huo, Umoja huo umetangaza kuwa, wabunge wa kambi ya upinzani bungeni wamekubaliana kuchanga kila mmoja Shilingi 300,000 kwa ajili ya familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo. Pia wamekubaliana Jumamosi ya Novemba 21, wote watakwenda kuungana na viongozi wengine wa kitaifa kumzika hayati Mawazo aliyeuliwa na watu wasiojulikana siku chache zilizopita.
No comments:
Post a Comment