Wednesday, 18 November 2015

KENYATTA: MGOGORO WA BURUNDI UTATULIWE

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito wa kuanza mazungumzo yenye lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. 
Rais Kenyatta amemtaka Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuziita katika meza ya mazungumzo pande zote zinazohusika na mgogoro huo ili kuzuia nchi hiyo isije ikatumbukia katika vita vya ndani. 
Rais wa Kenya amebainisha kwamba, Rais Nkurunziza ana uwezo wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo. Amesema amani na utulivu nchini Burundi ndio jambo muhimu kwa nchi hiyo. 
Wakati Rais Uhuru Kenyatta akitoa wito huo, wapinzani nchini Burundi wanaituhumu serikali ya Rais Nkurunziza kwamba, inafanya mauaji ya kupanga dhidi ya wapinzani. 
Katika upande mwingine jamii ya kimataifa imeendelea kuonyesha wasiwasi wake kutokana na kuendelea machafuko na mauaji nchini Burundi na kuonya juu ya uwezako wa kutokea mauaji ya kimbari kama yale yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. 
Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi ulianza tarehe Aprili mwaka huu baada ya chama tawala cha nchi hiyo cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Nkurunziza kugombea kwa muhula wa tatu mfululizo. 
Wapinzani nchini humo wanasema kuwa hatua hiyo ya Rais Nkurunziza ilikiuka katiba ya nchi pamoja na makubaliano ya Arusha, Tanzania.

No comments:

Post a Comment