Friday, 6 November 2015

CRISIS GROUP YATOA TAHADHARI VITA VYA NDANI BURUNDI

Kundi la kimataifa la Crisis Group limetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Kundi hilo limetangaza leo kuwa hali ya mamboya Burundi inatia wasiwasi.
Crisis Group limebainisha kuwa, Burundi inakabiliwa na duru mpya ya machafuko na kwamba upo uwezekano wa kuibuka vita vya ndani nchini. Kundi hilo la kimataifa linalojishugulisha na hali ya migogoro limeongeza kuwa, jeshi ni chombo pekee kinachoweza kukomesha hali hiyo huko Burundi, hata hivyo limesema, usuluhishi wa kidiplomasia unahitajika sasa ili kuiepusha Burundi kutumbukia kwenye vita vya ndani. Hii ni katika hali ambayo, watu wanne waliuawa katika mitaa miwili ya Bujumbura siku ya Jumatano. Mauaji ya mara kwa mara katika mji mkuu Burundi yamezusha wasiwasi mkubwa na kuwafanya baadhi ya raia wa mji huo kukimbilia katika nchi jirani za Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

No comments:

Post a Comment