Friday, 6 November 2015

ISRAEL YAMPIGA RISASI 50 MWANAMKE WA KIPALESTINA

  Katika kile kinachoonekana ni kuendeleza wimbi la hujuma zake za kikatili, vikosi vya utawala haramu wa Israel vimemuua mwanamke wa Kipalestina kwa kumfyatulia risasi 50, katika mji wa al-Khalil, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kadhalika Wapalestina wengine wawili waliokuwa katika eneo la tukio hilo wamejeruhiwa vibaya. Haya yanajiri siku chache baada ya jeshi katili la Israel kumpiga risasi na kumuua kijana wa Palestina katika kituo cha magari cha Jalama katika mji wa Jenin, katika Ukingo wa Magharibi. Makumi ya Wapalestina wameuawa kwa risasi ya utawala huo wa Kizayuni wakishiriki Intifadha ya 3 ya kulinda Quds Tukufu. 
 
Aidha Wapalestina zaidi ya 2600 wamepigwa risasi na askari wa Israel katika mwezi uliopita pekee katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

No comments:

Post a Comment