Thursday, 19 November 2015

RAIA WA MEXICO WAIHAMA MAREKANI

Rais wa Mexico Pena Nieto
Kutokana na Utafiti ulioendeshwa nchini Marekani unaonyesha raia wengi wa Mexico wanaondoka kwenye taifa hilo kubwa zaidi ulimwenguni ukilinganisha na idadi ya wanaoingia nchini humo,tofauti na hali ilivyokuwa nusu karne iliyopita.

MAGAIDI WALIJIFANYA WAHAMIAJI UFARANSA

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls.
Waziri mkuu wa Ufaransa,Manuel Valls, amesema kwamba watu wanaohusishwa na kundi la Islamic State ambao walitekeleza shambulizi mjini Paris wiki iliyopita,ambalo liligharimu uhai wa watu mia moja na ishirini na tisa,waliingia nchini humo kwa mgongo wa sakata la uhamiaji barani ulaya na kuzamia nchini Ufaransa bila kugundulika.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza katika runinga ya taifa hilo na kwamba wahusika wengine wa ugaidi walikuwemo katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji mapema.

Waziri huyo aliongeza kuwa haikufahamika mara moja kwamba kulikuwa na makundi ya namna hiyo kwa ukubwa wake ,ama mshukiwa Salah Abdeslam, ambaye ndiye hasa kielelezo cha mwanamume anayesakwa zaidi kimataifa na haikujulikana kama alikuwa Ubelgiji ama Ufaransa.

ALIYEPANGA MASHAMBULIO PARIS AUAWA

Abaaoud
Abaaoud anadaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129
Mwendesha mashtaka nchini Ufaransa amethibitisha kwamba mwanamume aliyetuhumiwa kupanga mashambulio ya Paris aliuawa kwenye operesheni ya jana.
Abdelhamid Abaaoud ndiye aliyekuwa akisakwa na polisi waliovamia nyumba moja katika mtaa wa Saint Denis, kaskazini mwa Paris jana.

WAZIRI MKUU WA TANZANIA 2015-

Majaliwa aidhinishwa kuwa waziri mkuu Tanzania

Mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameidhinishwa na Bunge la Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa Tanzania. Bw Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351 zilizopigwa, baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye aliyekuwa amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli awe Waziri Mkuu.

Wednesday, 18 November 2015

KENYATTA: MGOGORO WA BURUNDI UTATULIWE

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito wa kuanza mazungumzo yenye lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. 
Rais Kenyatta amemtaka Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuziita katika meza ya mazungumzo pande zote zinazohusika na mgogoro huo ili kuzuia nchi hiyo isije ikatumbukia katika vita vya ndani. 

UKAWA: MAGUFULI ATATUE KWANZA MASUALA YA ZANZIBAR

Viongozi wa UKAWA wakizungumza na waandishi wa habari
  Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA nchini Tanzania, wamesema kuwa, wamemwandikia barua Spika wa Bunge la nchi hiyo, Job Ndugai vikitaka kujua uhalali wa Rais John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge kabla ya kutangazwa matokeo rais wa Zanzibar.

UFARANSA YAWAUA WAPIGANAJI 33 SYRIA

wapiganaji wa islamic state mjini Raqqa

Mashambulio ya Ufaransa na mataifa mengine dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa nchini Syria siku ya jumapili yamewauwa takriban wapiganaji 33,wanaharakati wamesema.

POLISI WAVAMIA WASHUKIWA WA MASHAMBULIO PARIS


Maafisa walizingira sehemu ya mtaa wa Saint Denis wakisaka washukiwa wa mashambulio ya Ijumaa

Washukiwa wawili wamefariki baada ya maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini mwa Paris, wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.

Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea mapema asubuhi kwenye mtaa huo. Operesheni hiyo inadaiwa kumlenga mwanamgambo wa Islamic State Abdelhamid Abaaoud ambaye amedaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129.

Friday, 6 November 2015

CRISIS GROUP YATOA TAHADHARI VITA VYA NDANI BURUNDI

Kundi la kimataifa la Crisis Group limetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Kundi hilo limetangaza leo kuwa hali ya mamboya Burundi inatia wasiwasi.

ISRAEL YAMPIGA RISASI 50 MWANAMKE WA KIPALESTINA

  Katika kile kinachoonekana ni kuendeleza wimbi la hujuma zake za kikatili, vikosi vya utawala haramu wa Israel vimemuua mwanamke wa Kipalestina kwa kumfyatulia risasi 50, katika mji wa al-Khalil, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kadhalika Wapalestina wengine wawili waliokuwa katika eneo la tukio hilo wamejeruhiwa vibaya.

ICC YATAKA KUKABIDHIWA SEIFUL ISLAM GADDAFI

 
 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake mjini The Hague Uholanzi imeitaka serikali ya Libya yenye makao yake Tripoli imkabidhi kwa mahakama hiyo Saiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa dikteta wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi. 

MAHAKAMA YAFUTA NYONGEZA ZA MISHAHARA YA WALIMU KENYA


Mgomo walimu
 Mahakama ya masuala ya wafanyakazi ilikuwa imeagiza walimu walipwe nyongeza ya asilimia 50-60 lakini Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imebatilisha nyongeza ya mishahara ya hadi asilimia 60 ambayo walimu wa shule za serikali walikuwa wamepewa na Mahakama ya Mizozo ya Wafanyakazi.

MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HAZINA KUU

Magufuli
Rais mpya wa Tanzania John Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Hazina Kuu siku moja tu baada yake kuapishwa.