Msemaji
wa umoja huo , Ebba Kalondo, amesema toni la matamshi hayo lilikera
hata zaidi ikikadiriwa idadi ya Waafrika waliouzwa kama watumwa
Marekani.
Umoja huo unataka rais Trump aombe msamaha.
Inadaiwa
kwamba rais Trump alitoa matamshi hayo dhidi ya Africa, Haiti na
Elsavador kwenye ikulu ya White house katika mkutano na wabunge wa
congress.
Baadaye rais Trump alikana kutoa matamshi hayo.
Matamshi hayo yamekashifiwa na wengi, likiwemo shirika la kimataifa kuhusu haki za binadam.
Siku ya IJumaa bwana Trump alituma ijumbe wa Twitter
akisema kwamba lugha aliyotumia wakati wa mkutano wake na wabunge wa
Congress ili kuzungumzia swala la uhamiaji ilikuwa ngumu.
Lakini aliongezea kwamba maneno anayoshutumiwa kutoa sio lugha aliyotumia.
Umoja wa Afrika ulisema nini?
''Matamshi yalitolewa na Trump hayana heshima ya tofauti iliopo na haki za kibinaadamu''.
Uliongezea:
Huku tukionyesha kushangazwa kwetu , Umoja wa Afrika unaamini pakubwa
kwamba utawala mpya wa Marekani haulielewi bara la Afrika na watu wake.
''Kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya utawala wa Marekani na mataifa ya Afrika''.
No comments:
Post a Comment