Friday, 8 April 2016

WACHINA KWA KUKWEPA KULIPA KODI



Mfanyabiashara Raia wa Kichina, Huifang Ma akiwa chini ya ulinzi wa Polisi katika Mahakama ya mwanzo Ilala jijini Dar es Salaam jana kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi. Picha na Venance Nestory
 Raia wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.


Jun na Ma, ambao wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs pamoja na kushindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment